KWA NINI USILE TENA MKATE MWEUPE KUANZIA LEO?

0 coment



Mkate ndiyo chakula kikuu cha kila siku cha
familia nyingi duniani, hasa sehemu za mijini
na ndiyo chakula kinachotumika na watu wa
rika zote, wakubwa kwa wadogo, lakini ni
wangapi tunajua kuwa mkate mweupe,
ambao ndiyo chaguo namba moja la familia
nyingi, ni hatari kwa afya zetu?
Kuna msemo maarufu wa Kiingereza
kuhusu mkate mweupe usemao: The
Whiter the Bread, the Quicker You are Dead!
kwa tafsiri isiyo rasmi, msemo huu
unamaanisha kuwa ‘kadiri unavyopenda
kula mkate mweupe, ndivyo utakavyokufa
haraka!’ Amini, usiamini, mkate mweupe siyo
mzuri kwa afya yako!
Inawezekana kabisa habari hii
isikufurahishe, lakini kama kweli unataka
kuboresha afya yako, unapambana na suala
la kupunguza unene, unataka kujiepusha na
hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari
(Type II), ugonjwa wa moyo au saratani ya
tumbo, basi huna budi ya kuachana na mkate
mweupe.
Kama tulivyosisitiza kila mara katika makala
zetu nyingi za nyuma kuwa vyakula vyote
vitokanavyo na nafaka zilizokobolewa vina
hasara zaidi kiafya kuliko faida, mkate
mweupe nao ni miongoni mwa vyakula
hivyo.

KWA NINI USILE MKATE MWEUPE?
Kama ujuavyo, mkate unatengenezwa
kutokana na ngano na mkate mweupe
unatokana na unga wa ngano iliyokobolewa
na kuondolewa virutubisho vyake muhimu
vya asili ambavyo huwa muhimu katika
uimarishaji wa mfumo wa usagaji na
umeng’enyaji chakula tumboni (Digestive
system and metabolism).
Ili unga uwe mweupe, ngano baada ya
kukobolewa husafishwa kwa mashine
maalumu kwa kutumia kemikali na joto kali,
kitendo ambacho huondoa kabisa
virutubisho vinavyoweza kuwemo kwenye
nafaka na hivyo kuiacha punje ya ngano
ikiwa nyeupe na kubaki makapi.
Makapi hayo, baadaye husagwa na kuwa
unga safi na mweupe ambao hutayarishwa
kabla ya kutengenezwa mkate kwa kupitia
hatua mbalimbali, ikiwemo hatua ya
kuwekewa hamira ili uumuke, kuongezewa
sukari pamoja na chumvi ili kuongeza ladha.

MADHARA YANAYOWEZA KUKUPATA KWA
KULA MKATE MWEUPE
Madhara ya kwanza unayoweza kuyapata
kwa kupenda sana kula mkate mweupe ni
ugonjwa wa kisukari. Utafiti unaonesha
kuwa mkate au chakula chochote
kilichotengenezwa kutokana na unga
mweupe kina kiasi kingi cha wanga ambao
husababisha kuongezeka sukari mwilini.
Madhara mengine yatokanayo na mkate
mweupe ni kuongezeka kwa lehemu (bad
LDL cholesterol) kwenye damu, hali ambayo
inaweza kusababisha presha au magonjwa
ya moyo yatokanayo na kusinyaa au kuziba
kwa mishipa ya damu.
Madhara hayajaishia hapo, mengine
yanayoweza kukupata ni tatizo la ukosefu
wa choo kwa muda mrefu. Mkate mweupe
huchangia kuvuruga mfumo wa
umeng’enyaji wa chakula tumboni
(metabolism). Mwili unapokuwa hauna
virutubisho vya kutosha, usagaji na uondoaji
wa sumu mwilini huwa wa shida na uchafu
unaporundikana tumboni kwa muda mrefu
bila kutoka, husababisha kansa ya tumbo!
ULE NINI BADALA YA MKATE?
Kuna aina nyingine ya mkate ambayo ndiyo
unayopaswa kula, mkate huo ni BROWN
BREAD au MKATE MWEUSI kama
unavyojulikana na wengine. Mkate huu
hutengenezwa kutokana na ngano
isiyokobolewa hivyo kuwa na virutubisho
vyake asilia vinavyohitajika mwilini na kuwa
na faida zitakazokuepusha na kupatwa na
madhara yaliyotajwa hapo juu. Mkate huu
hauna sukari wala chumvi, hivyo kuwa bora
zaidi kwa afya yako. Kama kweli unajijali,
utaacha kula mkate mweupe na kuanza kula
huu mweusi leo!

Share this article :

Chapisha Maoni

 
Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved